#bongomovies News|SILVANUS MUMBA KUJA KIVINGINE NA NURU

Muandaaji na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania ndugu Silvanus C. Mumba, hivi karibuni alitambulisha kazi yake ya pili, ikiwa ni muendelezo wa Safari yake katika utume wa Uimbaji wa Injili Tanzania, Wimbo alioutambulisha unaitwa NURU, ambao unabeba jina la Albam yake.

Silvanus mumba

“Nimejitoa kwa ajili ya kuhakikisha nahubiri Injili kwa njia mbalimbali ikiwa katika filamu , muziki , njia yoyote ya sanaa ambayo Mungu kanipa kipaji katika sanaa,”alisema Mumba.

Amesema Albam itazinduliwa Mwezi March 2017 hivyo washabiki wake wa Filamu na Muziki wa Injili Tanzania na Nje ya Tanzania wampe suport kubwa katika kulifanikisha hilo… anasema hajawaangusha katika Albam hiyo.

Mtumishi huyo wa Mungu anasema kuwa yupoa katika maandalizi makubwa ya uzinduzi wa albam hiyo ambayo baadae atatengeneza filamu kubwa yenye sound track kupitia nyimbo za albam ya Nuru.

 

 

filamu central

444 total views, 2 views today

Leave a Reply

Your email address will not be published.