#bongomovies News|SERA YA FILAMU NDIO MWAROBAINI WA MATATIZO YA FILAMU- MH. NAPE

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape M Nnauye amesema kuwa vita dhidi ya maharamia wa filamu vina changamoto nyingi sana kulingana na mkanganyiko wa sheria za sasa kwani kuna mwingiliano ambao hautoi adhabu stahili kwa waharifu lakini anaamini upatikanaji wa Sera ya Filamu ndio dawa.

Nape Nnauye

Bi.Joyce Fissoo

“Tunajitaidi sana katika kupambana na maharamia wa kazi za filamu lakini sheria bado hazina nguvu au haziendani na kosa, mtu anakamatwa na faini haiendani kabisa na thamani mwarobaini wa wezi hawa ni Sera ya Filamu,”

Mh. Nape pia alisikitishwa na tabia za baadhi ya wasanii kutengeneza maneno ya uongo badala ya kupigania kupambana na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wizara yake kuliko kusema maneno yanayokatisha tamaa pale mtu anayetumia nguvu zake na pesa kumzushia maneno.

Waziri aliyasema hayo baada ya kuzushiwa maneno kuwa wauzaji wa filamu za nje wamempa hongo ya pesa kupitia Mbunge wa Ilala ili waendelee kuuza filamu bila stempu maana yake hazilipi kodi kama kazi za ndani Mh. Nape akiongea kwa kujiamini alisema ni muhimu kufanikinisha Sera ya filamu ambayo tayari wizara yake inafanya kazi usiku na mchana.

Bodi ya filamu imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sera ya filamu inapatikana kwa kushirikisha wadau wa tasnia ya filamu inapatikana na imekuwa katika mchakato na mafanikio yanaonekana kwani tayari watalamu wa Sera ya Filamu walishakutana Bagamoyo na kukamilisha hatua muhimu.

384 total views, 4 views today

Leave a Reply

Your email address will not be published.