#bongomovies News|DUDE AMSIFIA MKEWE EVA DUDE KWA NIDHAMU

Eva dude, Kulwa Kikumba

HARAKATI za wanawake ambao kila uchwao wameonekana wakijaribu kudai haki zao kupinga mfumo dume pale mwigizaji na muongozaji mahiri katika tasnia ya filamu Kulwa Kikumba ‘Dude’ pale ambapo amejikuta akimuomba msamaha mkewe Eva siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake huku akikiri kuwa amekuwa kero kwake.

Eva Dude

“Kama unampenda mkeo kwa dhati utafanya ninalofanya mimi , ni kweli mke wangu amekuwa mvumilivu sana juu yangu anasoma kashifa zinazoandikwa juu yangu na matatizo mengi lakini hakuwahi kuniacha wala kugombana nami,”alisema Dude.

Dude aliyasema hayo akimpongeza mke wake katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake akisema kuwa mkewe Eva Kulwa amekuwa ni mke mwenye subira asiye na papara hata anaposikia jambo kuhusu mumewe naye Dude anakiri kuomba msamaha na kumpongeza mkewe kama mama bora kwa familia.

416 total views, 2 views today

Leave a Reply

Your email address will not be published.